IQNA

Spika wa Bunge la Iran atoa mkono wa pole kufuatia kuuawa shahidi maafisa wa 'Sepah'

13:19 - November 13, 2011
Habari ID: 2221687
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) ya Iran ametoa mkono wa pole kufuatia kuuawa shahidi maafisa kadhaa wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu 'Sepah' katika mlipuko wa ghala la silaha pambizoni mwa jiji la Tehran siku ya Jumamosi.
Dakta Ali Larijani ameelezea kusikitishwa kwake na kuaga dunia maafisa kadhaa wa 'Sepah' akiwemo Meja Jenerali Hassan Tehrani Moqaddam, mkuu wa Taasisi ya Jihadi ya Kujitosheleza katika kikosi hicho.
Watu 17 waliepoteza maisha yao kufuatia mlipuko uliotokea jana katika ghala la silaha la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu magharibi mwa mji mkuu wa Iran, Tehran.
Mkuu wa uhusiano wa umma katika IRGC Luteni Generali Ramezan Sharif amesema watu wengine 16 wamejeruhiwa katika mlipuko huo uliotokea karibu saa saba kamili mchana kwa saa za Tehran. Imearifiwa kuwa mlipuko huo ulitokea wakati silaha zilipokuwa zikibebwa kuelekezwa eneo la oparesheni. Uchunguzi kuhusu chanzo cha mlipuko huo umeanza.
897531

captcha