IQNA

Wasiwasi wa Israel kuhusu ongezeko kubwa la Mashia katika jeshi la Lebanon

16:59 - November 13, 2011
Habari ID: 2221980
Gazeti la utawala wa Kizayuni wa Israel na Maariv limeripoti kuwa utawala huo una wasiwasi mkubwa kutokana na ongezeko kubwa la Mashia wanaoiunga mkono Hizbullah katika jeshi la Lebanon.
Gazeti la Maariv limeandika kuwa makamanda wa jeshi la Israel katika eneo la kaskazini wana wasiwasi mkubwa kuhusu ongezeko la idadi ya Mashia wanaoiunga mkono Hizbullah katika jeshi la Lebanon katika miaka ya hivi karibuni.
Vyombo vya kijeshi huko Israel vimetangaza kuwa baada ya kufutwa sheria ya wajibu wa kuhudumu katika jeshi hapo mwaka 2006, idadi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia imeongeza sana katika jeshi la Lebanon.
Limeongeza kuwa kinyume chake idadi ya Wakristo katika jeshi la Lebanon imepungua huku idadi ya maafisa wa ngazi za juu wa madhehebu ya Shia katika jeshi la Lebanon ikiongeza na kufikia asilimia 40.
Maariv limeandika kuwa Mashia wanaohudumu katika jeshi la Lebanon wamewekwa karibu na mpaka wa nchi hiyo na utawala ghasibu na Wakristo katika eneo la katikati mwa nchi hiyo. 897732


captcha