Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria Ammar Belani amesema kuwa kila nchi ina uhuru wa kuchukua maamuzi kuhusu wito huo wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na kwamba hilo ni suala la ndani la kila nchi. Amesema Algeria haikubaliani na uamuzi huo.
Amesisitiza kuwa Algeria ni nchi inayojitawala na inayochukua maamuzi yake kwa uhuru na wala haikubaliani na wito wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuhusu Syria.
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu waliokutana jana mjini Cairo Misri walitaka kusimamishwa uanachama wa Syria katika jumuiya hiyo, suala ambali lilipingwa na nchi za Yemen na Lebanon huku Iraq ikijizuia kupiga kura. 897895