IQNA

Waislamu wa New York waandamana kupinga ukandamizaji wa polisi

16:08 - November 19, 2011
Habari ID: 2224790
Mamia ya Waislamu wa jiji la New York nchini Marekani waliandamana jana wakipinga harakati za kijasusi zinazofanywa na polisi ya nchi hiyo dhidi ya raia Waislamu.
Idadi kubwa ya waandamanaji hao walikuwa wanafunzi Waislamu wa vyuo vikuu ambao wanalalamikia ujasusi unaofanywa kwa kipindi kirefu sasa na polisi ya Marekani dhidi ya raia Waislamu na bila ya sababu yoyote.
Ripoti zinasema kwamba polisi ya Marekani imekuwa ikifanya ujasusi katika masuala ya Waislamu katika misikiti, mahoteli, makazi ya Waislamu na kwenye vyuo vikuu.
Waandamanaji hao walitekeleza swala ya Ijumaa katika Medani ya Foley (Foley Square) katika mtaa wa Manhattan na kusisitiza juu ya udharura wa kutambuliwa Waislamu kama sehemu ya jamii ya Marekani na si maadui wa nchi hiyo. 900803
captcha