Kituo cha habari cha Courrierinternational kimeripoti kuwa baada ya kutolewa matokeo ya kura ya maoni ya taifa kuhusu ongezeko la ubaguzi nchini Finland, Rais wa nchi hiyo amewataka viongozi wa kisiasa na wananchi kukabiliana na wimbi la kueneza hujuma dhidi ya Uislamu na harakati za kibaguzi nchini humo.
Amekituhumu chama cha Vrais Finlandais (Wafindand Halisi) kuwa ndicho kinachoeneza ubaguzi nchini humo na amewataka wanachama wake kueneza amani na maelewano badala na kuhubiri fikra za kibaguzi.
Gazeti la Helsingin Sanomat la Finland limeandika kuwa kwa mujibu wa matokeo ya kura ya maoni iliyofanyika nchini humo, asilimia 12 ya Wananchi wa Finland wanaunga mkono fikra na itikadi za kibaguzi na wanasisitiza kwa nguvu zote juu ya kukabiliana na Uislamu na Waislamu na kujiona kuwa wao ni bora kuliko watu wa nchi nyingine. 900572