Askari hao wa Saudia mapema leo walimpiga risasi kijana huyo katika moja ya mitaa ya Qatif na kumjeruhi vibaya.
Vyombo vya usalama vya Saudi Arabia vimemchukua kijana huyo aliyekuwa amepotewa na fahamu kutokana na kutokwa damu kwa wingi na kumpeleka sehemu isiyojulikana.
Askari usalama wa Saudia pia walifyatua risasi ovyo katika mtaa wa Imam Ali (as) katika mji wa Qatif wenye raia wengi wa madhehebu ya Shia huko mashariki mwa Saudi Arabia.
Jeshi la Saudia limekuwa likivamia makazi ya Mashia wa mji huo mara kwa mara na kuzusha hofu na wasiwasi kati ya raia. 900868