Katika mjadala mkali uliorushwa hewani na kanali ya Marekani ya MSNBC, Larijani aliongeza kuwa utawala ghasibu wa Israel ndio chanzo cha matatizo yote Mashariki ya Kati.
Larijani pia amesema kuwa Marekani ndio muungaji mkono mkubwa zaidi wa ugaidi wa kiserikali duniani. Larijani amesisitiza kuwa miradi ya kuzalisha nishati ya nyuklia nchini Iran inafanyika kwa uwazi na kwamba Iran haina lengo la kuzalisha silaha hatari za nyuklia kwani hilo linaenda kinyume na mafundisho ya Kiislamu.
Dakta Larijani amesema Marekani inajaribu kuichafulia jina Iran kwa sababu Tehran ina uhusiano mzuri na nchi zote jirani.
900888