Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, wanachama wa Harakati ya Ikwanul Muslimin tawi la Libya baada ya kumalizika kikao chao walimteua Bashir al Kabti kutoka Benghazi kuwa kiongozi na kuchukua mahala pa Suleiman Abdulqadir.
Aidha katika kikao hicho cha siku tatu kilichofanyika Benghazi, mji uliokuwa chimbuko la mwamko wa watu wa Libya, Harakati ya Ikwanul Muslimin tawi la Libya iliteua wanachama wapya wa baraza lake la ushauri.
Kiongozi mpya wa Ikwanul Muslimin Libya amewaambia waandish habari kuwa, baada ya miaka 25 ya kuendesha harakati mafichoni, leo wanaharakati wa Kiislamu Libya wako tayari kukabiliana na changamoto mpya.
902344