IQNA

Mwakilishi wa UN azuru Haram ya Imam Ali (as), Najaf

17:48 - November 21, 2011
Habari ID: 2226383
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Martin Kobler amezuru Haram ya Imam Ali bin Abi Twalib (as) katika mji mtakatifu wa Najaf nchini humo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Darul Qur'an Kariim katika mkoa wa Dhiqar nchini Iraq Raad Adnan amesema, baada ya kuzuru Haram na kaburi la Imam Ali bin Abi Twalib (as), Martin Kobler amekutana na kufanya mazungumzo na Ayatullah Ali Sistan ambaye ni kiongozi wa ngazi za juu wa kidini nchini Iraq.
Amesema kuwa ziara ya mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq katika kaburi na Haram ya Imam Ali (as) imeakisiwa sana na vyombo vya habari. 902665


captcha