IQNA

Mjumbe wa UN nchini Iraq:

Lengo la kukutana na Ayatullah Sistani ni kufaidika na miongozo yake

17:11 - November 22, 2011
Habari ID: 2227114
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Martin Kobler amesema kuwa lengo la kukutana kwake na kiongozi mkuu wa kidini wa Iraq Ayatullah Ali Sistani ni kutaka kupata nasaha na miongozo yake.
Martin Kobler alizuru Haram ya Imam Ali bin Abi Twalib katika mji mtakatifu wa Najaf jana na kukutana na Ayatullah Ali Sistani.
Mhariri Mkuu wa jarida la Asala Ahmad Abdul Jabbar amesema, baada ya kukutana na Ayatullah Sistan, Martin Kobler alizungumza na waandishi habari na kusema lengo la safari yake mjini Najaf lilikuwa kuzuru Haram ya Imam Ali bin Abi Twalib na kuadhimisha mji huo mtakatifu na nafasi yake ya kimaanawi.
Katika mazungumzo yake na waandishi habari mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa alichunguza matatizo ya kisiasa, kijamii na masuala ya ustawi ya Iraq na vilevile hali ya baada ya kuondoka askari vamizi wa Marekani nchini humo. 903262

captcha