Maonyesho hayo yanasimamiwa na Taasisi ya Dini Tatu za Mbinguni yaani Uislamu, Ukristo na Uyahudi ya London kwa shabaha ya kutumia sanaa ili kuwahamasisha wafuasi wa dini mbalimbali kushirikiana zaidi.
Maonyesho hayo ambayo yataendelea kwa kipindi cha wiki mbili yatakuwa na kazi za wasanii Waislamu, Wakristo, Wayahudi na dini nyinginezo.
Maonyesho hayo pia yatakuwa na programu nyingine kama tamasha ya dini mbalimbali, siku ya familia na vikao vya wanawake wa dini za mbinguni. 903208