Ammar Mosa’edi Mkuu wa Kitivo cha Sayansi za Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Algeria amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa kongamano hilo limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya vyuo vikuu vya Tehran na Algeria.
Kongamano hilo limehutubiwa na wasomi sita kutoka Algeria pamoja na wanazuoni wa Kishia na Kisuni kutoka Iran, Tunisia, Syria, Misri, Sudan, Qatar na Amerika.
Kongamano hilo limejadili masiala kama vile, ‘dini na zama za utandawazi’, ‘nafasi ya fiqhi ya Kiislamu katika utandawazi’, na ‘familia na mwanamke katika utandawazi’.
902209