IQNA

Kituo cha Utafiti cha Uholanzi:

Wanawake wengi Waislamu wa Uholanzi wanavaa vazi la hijabu

20:15 - November 23, 2011
Habari ID: 2227930
Kituo kimoja cha utafiti nchini Uholanzi kimetangaza kuwa wanawake 6 kati ya kila 10 wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 35 nchini humo wanatumia vazi la hijabu bila ya kizuizi chochote.
Shirika la habari la Kuwait KUNA limeripoti kuwa kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliofanywa na Kituo cha Utafiti cha Motivation cha Uholanzi, wanawake 80 elfu wa Kiislamu wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 35 wanaishi nchini humo na sita kati ya kila kumi kati yao wanavaa vazi la hijabu ya Kiislamu.
Matokeo ya uchunguzi huo wa maoni pia yameonyesha kuwa asilimia 93 ya wanawake wa Uholanzi wanajihisi vizuri zaidi wakiwa na vazi la hijabu ya Kiislamu.
Matokeo hayo yanasema asilimia 70 ya wanawake Waislamu wa Uholanzi wanahisi kuwa vazi la hijabu ya Kiislamu limekubaliwa katika mazingira ya kazi zao na asilimia 62 kati yao wanasema waajiri wanafadhilisha kutomuajiri mwanamke anayetumia vazi la hijabu ya Kiislamu.
Vilevile matokeo hayo yanaonyesha kwamba wanawake wasiovaa hijabu ya Kiislamu wanasema sababu ya kutotumia vazi hilo ni kuwa hali hiyo inazidisha uwezekano wa kupata ajira kwa asilimia 41 na kuwapunguzia uwezekano wa kukabiliwa na ubaguzi wa kijamii kwa asilimia 20.
Waislamu wa Uholanzi ambayo ina jamii ya watu milioni 17, wanakaribia watu milioni moja. 904205
captcha