Mahakama ya mji wa Toronto ilitoa kibali cha kuruhusu vazi la hijabu ya Kiislamu kwa polisi wa kike miezi mitano iliyopita lakini idara ya polisi ya mji huo imechelewa kutekeleza amri hiyo hadi jana Jumanne.
Vyombo vya habari vya Canada vimeripoti kuwa polisi ya Toronto imewaruhusu rasmi polisi wa kike Waislamu kutumia vazi la hijabu la Kiislamu maofisini.
Mkuu wa polisi ya Toronto amesema idadi ya Waislamu inaongezeka siku baada ya siku katika mji huo na kwamba kuna udharura wa kutiliwa maanani matakwa yao.
Viongozi wa idara ya polisi ya Canada pia wana nia ya kuruhusu uuzaji wa bidhaa halali katika mikahawa ya polisi ya Toronto. 903871