IQNA

Wiki ya 'Ujue Uislamu' yaanza Uingereza

20:14 - November 23, 2011
Habari ID: 2227934
Wiki ya Ujue Uislamu ilianza jana katika mji wa Batley nchini Uingereza chini ya usimamizi wa jumuiya ya IMWS ya Waislamu wa India.
Kituo cha habari cha Batley News kimeripoti kuwa wiki ya Ujue Uislamu itaendelea hadi mwishoni mwa wiki hii.
Lengo la programu hiyo ya Ujue Uislamu ni kutayarisha fursa kwa watu kuujua Uislamu na Waislamu na kupambana na mienendo isiyokuwa sahihi kuhusu masuala hayo.
Miongoni mwa ratiba za wiki hii ni safari za kutembelea misikiti na shule za Kiislamu, semina zinazojadili suala la kuunganishwa Waislamu katika jamii ya Uingereza, mkutano wa mazungumzo ya viongozi wa Waislamu na Wakristo kuhusu njia za kuondoa hitilafu na ufahamu usiokuwa sahihi kuhusu dini ya Uislamu na Waislamu.
Vilevile kutakuwepo maenyesho na maeneo ya kuuza vitabu vya Kiislamu katika kipindi chote cha wiki hii. 904033


captcha