IQNA

Rais wa Italia ataka kufanyika mazungumzo kati ya dini mbalimbali

20:12 - November 23, 2011
Habari ID: 2227937
Rais Giorgio Napolitano wa Italia ameitaka Vatican kutayarisha uwanja wa kufanyika mazungumzo kati ya dini mbalimbali nchini Italia.
Rais wa Italia amesema katika mazungumzo yake na ujumbe wa Federesheni ya Makanisa ya Italia mjini Roma kwamba Vatican inalazimika kutayarisha uwanja mzuri wa kufanyika mazungumzo kati ya dini mbalimbali. Rais Giorgio Napolitano wa Italia ameongeza kuwa anamini mazungumzo kati ya dini mbalimbali hayapasi kufanyika katika uwanja wa kimatafa pekee bali yanapaswa kwanza kufanyika nchini Italia kati ya Kanisa Kikatoliki na dini nyinginezo.
Amesema anatarajia kuwa Bunge la Italia na wafuasi wa dini mbalimbali watatia saini hati ya melewano ambayo itakuwa utangulizi wa kustawisha mazungumzo kati ya duni mbalimbali. 903988

captcha