IQNA

Uwezekano wa kuundwa jumuiya ya vyombo vya habari vya Kiislamu duniani

15:20 - November 24, 2011
Habari ID: 2228174
Kuna uwezekano wa kuundwa jumuiya ya vyombo vya habari vya Kiislamu duniani, amesema mtaalamu wa masuala ya kisiasa.
Mojtaba Shakeri, Mwanachama wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Waliojitolea Vitani Iran ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya kisiasa katika mahojiano na IQNA amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaweza kuandaa mazingira ya kuundwa jumuiya kama hiyo.
Amesema madola ya kiistikbari na kibeberu yanatawala vyombo vya habari duniani na kuongeza kuwa, kwa sasa Wazayuni wanaamua kuhusu strategia na mwelekeo wa vyombo vikubwa vya habari. Kutokana na hilo wanapotosha ukweli na kuripoti matukio kwa njia inayojali maslahi yao haramu.
Shakeri amesema pamoja na kuwepo vyombo vya habari vyenye nguvu vya nchi za Magharibi, ujumbe wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wenye kutetea uadilifu na haki umeenea kote duniani.
Amesema kuundwa jumuiya ya vyombo vya habari vya Kiislamu duniani inaweza kusaidia vyombo vya habari vya Kiislamu kueneza habari kwa njia sahihi.
903577
captcha