IQNA

Sheikh wa al Azhar awaunga mkono waandamanaji Medani ya Tahrir

19:00 - November 26, 2011
Habari ID: 2229230
Mwakilishi wa Sheikh wa al Azhar nchini Misri jana alishiriki katika maandamano ya wananchi katika Medani ya Tehrir na kutangaza uungaji mkono wa kiongozi huyo wa kidini kwa wananchi wanaoandamana.
Hasan Shafi’i alikutana na waandamanaji wanaotaka utawala wa kijeshi wa Misri ukabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia katika Medani ya Tahrir na kuwaambia kuwa kiongozi huyo wa kidini anaunga mkono maandamano hayo.
Amesema Sheikh wa al Azhar anaunga mkono maandamano ya wananchi na anawaombea dua ili wapate ushindi.
Hii ni mara ya kwanza kwa Sheikh wa al Azhar ambaye anateuliwa na Rais wa Misri kuchukua msimamo unaopinga serikali, suala ambalo limewafariji wananchi wanaoandamana Medani ya Tahrir.
Mamilioni ya wananchi wa Misri walifanya maandamano makubwa jana Ijumaa katika Medani ya Tahrir ambayo yamepewa jina la ‘Ijumaa ya Shahidi’. Maandamano kama hayo pia yamefanyika katika miji mblimbali ya Misri. 905550

captcha