Msemaji wa kamati ya kampeni ya chama cha uadilifu na Usawa Hassan Lamrani amesema kuwa chama hicho kimepata ushindi mkubwa na kuviacha nyumba vyama vingine.
Hassan Daudi ambaye ni miongoni mwa viongozi wa chama hicho amesema kuwa kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa hadi sasa chaama cha Uadilifu na Usawa kimepata ushindi mkubwa katika miji mikubwa ya Moroco.
Daudi ameongeza kuwa chama hicho kimepata ushindi katika miji ya Casablanca, Rabat na Tanja.
Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Moroco al Tayyib al Sharqawi amesema asilimia 45 ya watu waliotimiza masharti wameshiriki katika zoezi la uchaguzi huo wa bunge. Ameongeza kuwa matokeo ya mwisho ya uchaguzi huo yatatangazwa kesho. 905263