Wakazi wa mji wa Qatif wanajitayarisha kwa ajili ya kuanza maombolezo ya siku kumi ya kukumbuka mauaji ya mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) Imam Hussein (as), na kuwepo askari wengi wa utawala wa kifalme wa Saudia katika mji wa Qatif ni aina fulani ya kuwatia woga na hofu wakazi wa mji huo.
Askari hao wa Saudia pia wamefunga barabara kuu za mji huo kwa ajili ya kudhibiti harakati za Waislamu wa madhehebu ya Shia.
Wakazi wa mji wa Qatif wamekuwa wakifanya maandamano ya kupinga siasa za kibaguzi wa utawala wa kifalme wa Saudia.
Vijana wa Qatif wamekuwa wakiandika nara mbalimbali katika kuta za mji huo kama ‘mauti kwa Aal Saud’ na ‘utawala wa Aal Saud utaporomoka’ ikiwa ni moja ya njia za kudhihirisha upinzani wao dhidi ya siasa za kibaguzi za watawala wa Saudi Arabia dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia. 905604