IQNA

Ayatullah Khamenei:

Njama za Magharibi za kukandamiza harakati za Kiislamu zitafeli

0:04 - November 28, 2011
Habari ID: 2230069
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa njama zinazofanywa na madola ya Magharibi kwa ajili ya kukandamiza na kupotosha mwamko wa Kiislamu katika eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika ni juhudi zilizogonga mwamba.
Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesisitiza kuwa harakati za Kiislamu za mataifa ya eneo hili bila ya shaka zitadumu na kusonga mbele na kwamba kuzidi kuwa macho wananchi kila uchao kutakata mikono ya mabeberu wa dunia mmoja baada ya mwingine, jambo ambalo linaashiria uwezo na kuzidi kuimarika dini tukufu ya Kiislamu katika siku za usoni. Ayatullah Khamenei ameyasema hayo leo hapa Tehran wakati alipokutana na mjumuiko mkubwa wa maelfu ya mabasiji wa maeneo yote ya Iran katika Chuo Kikuu cha Kijeshi cha Imam Ali A.S. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, mwamko wa Kiislamu katika eneo la Mashariki ya Kati, umeiathiri dunia na hasa Marekani na Ulaya na kwamba walimwengu wameshuhudia haraka mabadiliko makubwa yaliyotokana na mori wa harakati hizo za Kiislamu.
906362
captcha