IQNA

Wanaharakati wa haki za binadamu wa Saudia walaani jinai za utawala wa nchi hiyo

15:51 - November 28, 2011
Habari ID: 2230602
Wanaharakati 171 wa haki za binadamu katika mkoa wa Qatif nchini Saudi Arabia siku ya Jumamosi walitoa taarifa wakilaani vikali jinai zinazotekelezwa na utawala wa nchi hiyo dhidi ya Mashia.
Wamekosoa pia siasa na msimamo wa utawala huo unaodai kwamba Mashia wa Saudia wanahudumia na kutii tu viongozi wao wa kidini walio nje ya mipaka ya nchi hiyo. Wanaharakati hao wamelaani pia matukio ya hivi karibuni yaliyopelekea kuuawa na kujeruhiwa kwa watu kadhaa katika mkoa huo, jambo ambalo wanamesisitiza kwamba lilisababishwa na ukandamizaji pamoja na kiburi cha watawala wa nchi hiyo cha kutotekeleza matakwa ya kimsingi ya Mashia.
Kwa kutia saini taarifa hiyo, wanaharakati waliotajwa wamewataka askari usalama wa Saudia kuchukua tahadhari kubwa wanapokabiliana na malalamiko ya wapinzani na kujiepusha kutumia risasi hai dhidi ya waandamanaji wanaolalamikia siasa za utawala wa nchi hiyo.
Utumiaji nguvu wa askari usalama wa Saudia katika matukio ya hivi karibuni ulipelekea Mashia wanne kuuawa shahidi na wengine kadhaa kujeruhiwa katika makabiliano na askari hao waliotumia risasi hai dhidi ya waandamanaji wasiokuwa na silaha.
Taarifa hiyo ya wanaharakati imeutaka utawala wa Saudia ujiepushe kutekeleza siasa za ubaguzi wa kimadhehebu dhidi ya raia wake na pia kutotumia risasi hai dhidi ya waandamanaji wanaoandamana kwa njia za amani wakitaka kuheshimiwa haki zao za kimsingi. 906180
captcha