IQNA

Mwanaharakati wa Misri aonya juu ya udhibiti wa Mawahabi katika serikali ya nchi hiyo

16:21 - November 29, 2011
Habari ID: 2231412
Muhammad Ala Madhwi Abul Azayim, mwanazuoni mashuhuri wa Misri na mmoja wa waanzilishi wa Chama cha at-Tahrir cha nchi hiyo amesema kwamba suala la masalafi wa Kiwahabi kupata satuwa na ushawishi katika serikali ya nchi hiyo ni hatari kubwa.
Amesema iwapo masalafi watapata fursa hiyo ni wazi kuwa Misri itarejea nyuma katika zama za ujahilia.
Kwa mujibu wa gazeti la al-Ittihad linalochapishwa Imarati, Sheikh Abu Azayim amesema kuwa iwapo Mawahabi watapata ushawishi na kudhibiti serikali ya Cairo ni wazi kuwa nchi hiyo iterejeshwa nyuma miaka 5000 na kuishi katika giza la ujahilia. Amesema Mawahabi ni watu walio na misimamo finyu na ya kupindukia mipaka ambao hata hawapatani wao kwa wao na kwamba licha ya kuwakufurisha Waislamu wenzao hukufurishana wao kwa wao. Sheikh Abu Azayim amesema Masufi na Makopti wa Misri ni miongoni mwa watu wanaokufurishwa na Mawahabi.
Akibainisha zaidi historia ya usufi nchini Misri, Sheikh Abul Azayim amesema kuwa utawala wa kidikteta wa Hosni Mubarak ulitumia mbinu zote kudhoofisha harakati ya usufi katika jamii ya nchi hiyo.
Amesisitiza mwishoni kwamba Wasufi wa Misri ni miongoni mwa watu wa kwanza kabisa kuunga mkono mapinduzi ya Januari 25 dhidi ya utawala huo na kisha kuanzisha chama cha Tahrir ili kupigania haki zao za kisiasa na kijamii zilizokuwa zimekanyagwa na utawala huo wa zamani. 907164
captcha