IQNA

Waislamu Mashia Romania hawana msikiti

16:12 - November 30, 2011
Habari ID: 2232076
Waislamu wa madhehebu ya Shia walioko Romania wakiwemo Wairani 4000 hawana misikiti, amesema mkurugenzi wa Kituo cha Fiqhi ya Aimma At’har AS.
Hujjatul Islam Seyyid Javad Nurmusavi ambaye yuko Romania kushiriki katika mihadhara ya maombolezo ya Muharram iliyoandaliwa na Waislamu wa mdhehebu ya Shia amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa, Mashia ya Romania wamekodisha ukumbi kwa ajili ya maombolezo ya Muharram.
Amesema kila mwaka mwezi wa Muharram, Jumuiya ya Wapenzi wa Imam Hussein mjini Bucharest Romania huandaa vikao vya maombolezo ya kukumbuka tukio la kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS.
908459
captcha