Kwa mujibu wa takwimu za awali za uchaguzi huo, wagombea wa chama cha Uhuru na Uadilifu hadi sasa wamepata asilimia 40 katika majimbo mengi ya kupigia kura.
Muungano wa al Kutlatul Misriyya unafuatia kwa kuwa na asilimia 15 na chama cha An Nour kinashika nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 8. Chama cha al Wafdi kimeshika nafasi ya nne kwa kupata asilimia 5 ya kura zilizopigwa.
Awamu ya kwanza ya uchaguzi wa Bunge la Misri ilianza Jumatatu ya wiki hii na kumalizika jana Jumanne na matokeo yake yanatazamiwa kutangazwa hii leo.
Awamu ya kwanza ya uchaguzi wa bunge la Misri ambao ni wa kwanza wa kidemokrasia baada ya kung'olewa madarakani dikteta Hosni Mubarak, imefanyika katika mikoa 9 kati ya 27 ya nchi hiyo. Awamu ya pili itafanyika katika mikoa 18 iliyobakia. 908767