IQNA

Kongamano la amani na umoja kati ya Shia na Suni lafanyika Kashmir

15:17 - December 04, 2011
Habari ID: 2233885
Mashia na Masuni wa India walikutana jana Jumamosi huko Srinagar, mji mkuu wa jimbo la Jamu na Kashmir ili kujadili njia za kuimarisha amani na umoja kati yao.
Kwa mujibu wa tovuti ya newstrackindia kongamano hilo limefanyika kwa mnasaba wa kuwadia siku ya kuuawa shahidi Imam Hussein (as) mjukuu wa mtukufu Mtume (saw) katika tukio chungu na la huzuni la Ashura huko Karbala nchini Iraq.
Kongamano hilo lililoanza kwa kiraa ya Qur'ani Tukufu na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya wasomi, wanafikra na wanazuoni wa Kiislamu lilichunguza kwa kina maisha na mafunzo ya Imam Hussein (as) kwa umma wa Kiislamu kutokana na mapambano yake matukufu katika ardhi ya Karbala. Akizungumza katika kongamano hilo Bashir Nahwi, mmoja wa manazuoni wa India amesema kuwa kongamno hilo limefanyika kwa madhumuni ya kuimarisha uhusiano na udugu wa Kiislamu kati ya Waislamu wa Kishia na Kisuni. 910202
captcha