IQNA

Umoja wa Mataifa walaani shambulizi la kigaidi dhidi ya waomboleza Afghanistan

12:42 - December 08, 2011
Habari ID: 2235135
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na ujumbe wa taasisi hiyo nchini Afghanistan wamelaani milipuko ya mabomu iliyolenga Waislamu wa madhehebu ya Shia waliokuwa katika maombolezo ya kifo cha Imam Hussein (as) katika miji ya Kabul na Mazar Sharif na kuua makumi ya raia wasiokuwa na hatia yoyote.
Kituo cha habari cha Afghanpaper kimeripoti kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa amelaani milipuko ya mabomu iliyotokea nchini Afghanistan siku ya Ashura.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa Katibu Mkuu wa umoja huo analaani vikali mashambulizi ya kigaidi ya Afghanistan na ametuma salamu za rambirambi kwa familia zilizopatwa na msiba.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan pia umelaani mashambulizi ya kigaidi Jumanne iliyopita nchini Afghanistan.
Taarifa ya ujumbe huo imesema: Mashambulizi kama hayo hayawezi kukubaliwa kwa njia yoyote ile na wale wanaohusika na vitendo hivyo wanapaswa kujibu mashtaka ya kumwaga damu za watu.
Zaidi ya watu 60 waliuawa juzi katika siku ya Ashura wakiomboleza mauaji ya mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) katika miji ya Kabul na Mazar Sharif nchini Afghanistan. 911501
captcha