Mtu huyo mwenye umri wa miaka 33 alitiwa nguvuni jana akijaribu kuchoma moto kituo kingine cha Kiislamu.
Polisi ya Ufaransa imetangaza kuwa kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi uliofanyika, mtu huyo ambaye ni mwanachama wa kundi moja la kibaguzi hadi sasa amekwishashambulia vituo saba vya ibada vya Waislamu.
Polisi ya Ufaransa inafanya uchunguzi wa kutafuta wanachama wengine wa kundi la kibaguzi ambao yumkini wameshiriki katika kushambulia maeneo ya ibada ya Waislamu nchini humo.
Tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2011 hadi sasa misikiti na maeneo 24 ya ibada na misikiti ya Waislamu imeshambuliwa na makundi ya kibaguzi katika miji mbalimbali ya Ufaransa. Polisi ya nchi hiyo inalaumiwa kwa kuzembea au kupuuza mashambulizi kama hayo yanayolenga vituo na maeneo ya ibada ya Waislamu. 911408