IQNA

Ubalozi wa Misri nchini Iraq watiliana saini hati ya maelewano na Darul Qur'an ya Karbala

11:25 - December 12, 2011
Habari ID: 2237098
Ubalozi wa Misri nchini Iraq umetiliana saini hati ya ushirikiano na Darul Qur'an ambayo inafungamana na Haram ya Imam Hussein (as) katika mji mtakatifu wa Karbala kwa madhumuni ya kuimarisha shughuli za Qur'ani, dini na utamaduni.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Nun, hati hiyo ya ushirikiano ilitiwa saini kati ya Balozi Sharif Kamal Shahin wa Misri nchini Iraq na Abdul Mahdi Karbalai, Mkuu wa Haram ya Imam Hussein (as) mjini Karabala. Lengo la hati hiyo ya ushirikiano kama tulivyosema mwanzoni ni kuimarisha shughuli za utamaduni, dini na Qur'ani Tukufu katika nchi mbili hizo.
Sheikh Hassan al-Mansuri, Mkuu wa Darul Qur'an al-Karim amesema kuhusiana na suala hilo kwamba ana matumaini makubwa kwamba hati hiyo ya ushirikiano itaimarisha juhudi za umoja wa Kiislamu, kuvumiliana na kusameheana pamoja na mabadilishano ya kiutamaduni kati ya chuo cha Kidini cha al-Azhar na Kituo cha Kidini cha Najaf. Ameendelea kusema kuwa taasisi hizo mbili zina mipango ya kufanya maonyesho ya pamoja ya kidini na kiutamaduni ili kudhihirisha vipawa na uwezo wao katika nyanja hizo. Balozi Shahin pia alipata fursa ya kuzuru Haram ya Imam Hussein (as). 913563
captcha