Kituo cha habari cha Institut-imem kimeripoti kuwa kongamano hilo litasimamiwa na Taasisi ya Mediterania na Utafiti wa Kiislamu (IMEM). Mkutano huo utahudhuriwa na wasomi, wanafikra, wataalamu wa elimu jamii na wanazuoni wa kidini wa ndani na nje ya Ufaransa.
Ajenda kuu ya mkutano huo ni kuchunguza hali ya Waislamu wa Ufaransa, misimamo ya serikali ya Paris kuhusu matatizo yao na mitazamo mbalimbali kuhusu mafunzo ya Uislamu na mbinu za kutolewa mafunzo hayo katika jamii ya Ufaransa.
Baadhi ya wasomi wa Kiislamu wanaamini kwamba Ufaransa inataka kulazimisha 'Uislamu wa Kifaransa' unaotofautiana na thamani halisi za Kiislamu na unaopotosha itikadi za dini hiyo tukufu. 914001