IQNA

Kikao cha 'Mipaka ya Mazungumzo Baina ya Uislamu na Ukristo' chafanyika Paris

14:32 - December 13, 2011
Habari ID: 2237815
Wanafikra na wasomi wa Kiislamu na Kikristo wanakutana leo Jumanne mjini Paris, Ufaransa kwa madhumuni ya kuchunguza mipaka na pande mbalimbali za mazungumzo baina ya dini za mbinguni.
Kwa mujibu wa tovuti ya legaic, kikao hicho ambacho kimeandaliwa na Kamati ya Dini ya Taasisi za Familia za Ufaransa na Kundi la Urafiki kati ya Uislamu na Ukristo la Ufaransa kitawashirikisha wanafikra ambao watachunguza masharti, mazingira na mipaka ya kufanyika mazungumzo mazuri na ya kweli kati ya wafuasi wa dini tofauti za mbinguni ili kuwawezesha kuishi pamoja kwa amani.
Christophe Roucou, mkuu wa kitengo cha huduma za kitaifa kwa ajili ya uhusiano wa Kiislamu katika Taasisi ya Makasisi wa Ufaransa na Said Ali Kozai, mtaalamu wa masuala ya Kiislamu na mwanachama wa Kamati ya Dini ya Taasisi ya Familia za Ufaransa ni miongoni mwa wanafikra na wasomi mashuhuri walioalikwa kuhudhuria na kuzungumza kwenye kikao hicho.
Maryam Bu Raghba, Naibu Mkuu wa Kundi la Urafiki kati ya Uislamu na Ukristo anayesimamia kikao hicho atawasilisha matatizo na changamoto kadhaa zinazozuia kufanyika mazungumzo halisi kati ya wafuasi wa dini za Kiislamu na Kikristo na kuwasihi washiriki kutafua njia za kukabiliana na changamoto hizo. 914295
captcha