Katibu Mkuu wa OIC Ekmeleddin Ihsanoglu ameuambia ujumbe wa Gabon kwamba hii itakuwa mara ya kwanza kwa mkutano huo wa Mawaziri wa Habari wa nchi za Kiislamu kufanyika nchini humo.
Ujumbe huo wa Gabon umeeleza mipango na maandalizi yaliyofanyika hadi sasa kwa ajili ya mkutano huo.
Ujumbe huo pia umejadiliana na kubadilishana mawazo na maafisa wa ngazi za juu wa OIC kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu mkutano huo.
Mkutano huo utaanza tarehe 18 hadi 21 Aprili mwakani. 915504