IQNA

Maandamano ya Wairaki ya kutaka kuondolewa Munafiqeen nchini kwao

16:30 - December 17, 2011
Habari ID: 2240101
Maelfu ya Wairaki walifanya maandamano makubwa hapo jana Ijumaa wakitaka kundi la magaidi wa Munafiqeen walio na kambi yao katika ardhi ya Iraq waondolewe mara moja nchini kwao.
Kwa mujibu wa tovuti ya al-Alam, waandamanaji hao ambao walitoka matabaka mbalimbali ya kiutamaduni, kidini, wafugaji na wanasiasa wa Iraq walikusanyika katika Medani ya at-Tahrir mjini Baghad na kutaka magaidi hao wafukuzwe kutoka nchini kwao haraka iwezekanavyo.
Waandamanaji wametahadharisha dhidi ya njama za kundi hilo za kuwaua Wairaki na kuchochea fitina za kimadhehebu nchini Iraq. Wameitaka serikali ya Iraq kutosalimu amri mbele ya mashinikizo ya nchi za Ulaya na Marekani za kutaka magaidi hao wabakishwe Iraq.
Waandamanaji wametoa taarifa wakiitaka serikali ya Iraq kuwahukumu watenda jinai wote ambao mikono yao imejaa damu ya Wairaki. Waandamanaji wamesisitiza kwamba magaidi hao wanapasa kufukuzwa kwenye kambi ya Ashraf ambayo kwa sasa inaitwa Iraq Mpya na ardhi hiyo kurejeshewa wamiliki wake halisi ambao ni Wairaki.
Nuri Maliki Waziri Mkuu wa Iraq alisema siku ya Alkhamisi kwamba kundi la Munafiqeen ni kundi la kigaidi na kijinai ambapo uamuzi wa kulifukuza nchini Iraq hauwezi kubadilishwa. 916585
captcha