Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imesema hatua kama hizo haziwezi kukubalika na imewataka viongozi wa Israel kutekeleza wajibu wao wa kulinda raia wa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Palestina.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imeitaka pia Israel iwakamate na kuwafikisha mahakamani watu wanaoshambulia misikiti ya Wapalestina.
Mapema Alkhamisi iliyopita Wazayuni wenye misimamo mikali wa Israel walishambulia na kuchoma moto Msikiti wa al Nour katika kijiji cha Burqa katika mfululizo wa hujuma za walowezi wa Kiyahudi dhidi ya misiki na maeneo matukufu ya Kiislamu. 916938