Waandamanaji hao wametangaza upinzani wao mkubwa dhidi ya njama zinazofanywa na Israel za kupiga marufuku adhana katika misikiti ya Palestina.
Gazeti la Yediot Ahronot la Israel limeripoti kuwa washiriki katika maandamano hayo wamelaani ukiukaji wa sheria unaofanywa na utawala ghasibu wa Israel na vitendo vya walowezi wa Kizayuni vya kuvunjia heshima misikiti na maeneo ya ibada ya Waislamu.
Gazeti hilo pia limeripoti kuwa askari usalama wa Israel wamevamia nyumba ya Sheikh Khidhr Adnan ambaye ni miongoni mwa viongozi wa harakati ya Jihad Islami ya Palestina.
Rasimu ya sheria ya kupiga marufuku adhana katika misikiti ya Waislamu wa Palestina wanaoishi katika ardhi zilizokaliwa kwa mabavu na Israel mwaka 1948 iliwasilishwa bungeni na chama cha Yisrael Beiteinu kinachoongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Avigdor Lieberman. 917825