IQNA

Semina ya Fiqhi ya Kiislamu na Sheria za Kimataifa yafanyika Mauritania

15:16 - December 21, 2011
Habari ID: 2242696
Semina ya Fiqhi ya Kiislamu na Sheria za Kimataifa ilifanyika jana Jumanne huko Nouakchott, mji mkuu wa Mauritania kwa udhamini wa Kituo Kikuu cha Utafiti wa Kiislamu.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Mauritania, semina hiyo ambayo ilisimamiwa na Sayyid Ould an-Nueini, Waziri wa Masuala ya Kiislamu na Elimu wa Mauritania pia ilifanyika kwa ushirikiano wa Hilal Nyekundu ya nchi hiyo.
Semina hiyo imehudhuriwa na as-Sayyid Abideen Walad ak-Kheir, Waziri wa Sheria wa Mauritania, watafiti na wanachuo wa kituo kikuu kilichotajwa cha utafiti wa Kiislamu. Akizungumza katika semina hiyo, Waziri wa Masuala ya Kiislamu wa Mauritania amesema kuwa lengo la dini za mbinguni pamoja na sheria zinazobuniwa na mwanadamu ni kumsaidia kulinda usalama wake pamoja na kumuepusha na hatari zinazomkabili maishani.
Ahmad Ould Abah mmoja wa wasomi waliozungumza katika kikao hicho amesema kuwa mazungumzo ya kiutamaduni na kiustaarabu kwa ajili ya kumuhudumia mwanadamu ni moja ya malengo muhimu ya dini ya Kiislamu kwa madhumuni ya kuwaletea wanadamu wote saada ya humu duniani na huko Akhera. Amesema taasisi za kielimu na mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu yana jukumu muhimu katika kupunguza matatizo yanayoikabili jamii ya mwanadamu na hasa nyakati za vita. 919885
captcha