Kituo cha habari cha al Manar kimeripoti kuwa Katibu Mkuu wa Hizbullah amezungumza na kubadilishana mawazo na Mwenyekiti wa chama cha Ukombozi wa Kitaifa Michel Aun. Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na Waziri wa Nishati wa Lebanon Hussein Khalil na Wafiq al Safa ambaye ni miongoni mwa maafisa wa Hizbullah, kulitolewa ripoti kuhusu shughuli za chama cha Ukombozi wa Kitaifa.
Pande hizo mbili zimesisitiza juu ya umuhimu wa kuwepo ushirikiano kamili na kutumia vyema suhula zilizopo katika ushirikiano wa siku za usoni. 920135