Mkutano huo utasimamiwa na Msikiti wa al Fat'h baada ya Swala ya Magharibi ukiwashirikisha maulamaa wa Kiislamu, wataalamu wa masuala ya jamii na raia wa mji mkuu wa Ubelgiji.
Maulama na wataalamu wa masuala ya kijamii watajadili na kubadilishana mawazo kuhusu matatizo ya raia Waislamu katika nchi zisizo za Kiislamu na njia za utatuzi wa matatizo hayo.
Viongozi wa Msikiti wa al Fat'h wametangaza kuwa watu watakaohudhuria mkutano huo wanaweza kutoa mapendokezo yao kuhusu njia za utatuzi wa matatizo yao ili ziwasilishwe kwa viongozi wa serikali.
922152