Tovuti ya Muslim Congress imeripoti kuwa mkutano huo utafanyika tarehe Mosi hadi Pili Julai mwakani kwa nara ya Dunia Inasubiri Uadilifu, na Uadilifu Unamsubiri Mahdi (as).
Baadhi ya mambo yatakayojadiliwa katika kongamano hilo la kimataifa ni sifa za uadilifu wa Imam Mahdi (as), uadilifu bila ya uongozi wa Mwenyezi Mungu, sifa za wafuasi na masahaba wa Imam Mahdi (as), uadilifu mkabala wa usawa wa zama za sasa, utatuzi wa mporomoko wa kijamii, mwokozi aliyeahidiwa na uongozi wa Kiislamu katika zama hizi.
Kandokando ya kongamano hilo kutakuwapo na mijadala kuhusu mitazamo ya Shia, uhuishaji wa utambulisho wa Kiislamu na kadhalika.
Mkutano wa 7 wa kimataifa wa Waislamu wa Marekani ulifanyika mwaka jana chini ya anwani ya 'Imam Hussein (as) na Maana ya Uhuru katika Mtazamo wa Dini ya Mwenyezi Mungu.
Kongresi ya Waislamu wa Marekani ni jumuiya isiyo ya serikali inayoendeshwa kwa misaada ya Waislamu. 922850