IQNA

Binti Mfalme Basma Binti Saud:

Makundi yanayowakufurisha Waislamu yanaidhibiti Saudia

21:57 - December 27, 2011
Habari ID: 2246596
Binti Mfalme wa Saudi Arabia amesema kuwa nchi hiyo imekumbwa la wimbi la misimamo mikali, ujinga na makundi ya kuwakufurisha Waislamu na kwamba utawala wa nchi hiyo umo katika hali ya kuporomoka.
Kanali ya televisheni ya kimataifa ya al Alam imemnukuu Binti Mfalme Basma binti Saud bin Abdul Aziz akiwataka wananchi wa Saudia kuwajibika na kuiokoa nchi yao kutoka kwenye wimbi la watu wenye misimamo ya kuchupa mipaka, ujinga na misimao ya kisalafi ya kuwakufurisha Waislamu wengine.
Binti Mfalme Basma amesema iwapo maulamaa, kanali za televisheni na magazeti ya Saudi Arabia yana ushujaa wa kukutana naye, yuko tayari kufanya mazungumzo nayo katika uwanja huo.
Amesisitiza kuwa anazungumza kama raia wa Saudi Arabia na mmoja wa wana wa mmoja wa waasisi wa nchi hiyo na si kwa sababu za kipropaganda kama baadhi ya duru za serikali ya Riyadh zinavyodai.
Mapema mwezi Septemba Binti Mfalme Basma binti Saudi aliulaumu utawala wa kifalme Saudi Arabia kuwa umezama katika ufisadi. Basma ni mwana wa ndugu yake Mfalme Abdullah wa Saudia na mwanaharakati wa kijamii. 924020



captcha