IQNA

Tawakali huleta utulivu wa moyo

16:58 - December 29, 2011
Habari ID: 2247497
Wakati mwanadamu anapomtegemea Mwenyezi Mungu, huweza kufikia utulivu wa moyoni, amesema Sheikh Mohammad Abbaspour mwanasaikolojia mwandamizi nchini Iran.
Akizungumza na IQNA, Sheikh Abbaspouru ameongeza kuwa baraka za Mwenyezi Mungu daima huwashukia wale wenye imani na kuwasaidia kujikwamua kutoa katika hali ngumu.
Amesema kuwa kuishi maisha bora kunahitaji hulka njema, vitendo vyema na imani sahihi.
‘Vitendo ambavyo havina ikhlasi moyoni humzuia mwanadamu kupata afya ya kiakili. Aidha tabia ya kuwadhulumu wengine na kujidhulumu nafsi pia huathiri vibaya afya ya kiakili’, amesema.
Kuhusu suala la kumkumbuka Mwenyezi Mungu na utulivu wa moyo, Abbaspour ameashiria aya ya 28 ya Sura Ar-Raad isemayo: “Wale walioamini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutua!”. Sheikh Abbaspour amesema mtu mwenye afya ya kiakili hukataa kuwadhulumu wanadamu wengine na huheshimu haki za wengine.
Amesema kuwa muumini huyatizama masaibu maishani kama mtihani wa Mwenyezi Mungu na hivyo imani yake haitikiswi na matatizo hayo.
923113
captcha