IQNA

Mabeberu wana hofu na muungano wa mataifa ya Kiislamu

0:21 - December 31, 2011
Habari ID: 2248019
Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema Wamagharibi wana hofu na woga kutokana na mabadiliko yanayojiri sasa katika eneo la Mashariki ya Kati hususan muungamo wa mataifa ya Kiislamu.
Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa hapa jijini Tehran amesema kuwa wananchi wa Iran watatoa pigo jingine kwa maadui wakati watakaposhiriki kwa wingi kwenye uchaguzi wa bunge unaotarajiwa kufanyika Machi 2 mwaka ujao.
Ayatullah Ahmad Khatami amesema mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umejengeka juu ya msingi wa demokrasia na kwamba wananchi siku zote hufurahia kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kushiriki kwenye chaguzi mbalimbali.
Amekosoa wale wanaowataka wananchi kususia uchaguzi huo akisema kuwa wananchi wa Iran watapuuza kelele za watu hao.
Akiashiria matukio ya baada ya uchaguzi mkuu wa rais wa mwaka 2009, Ayatullah Khatami amesema taifa hili limejifunza mengi na haliko tayari kurudi katika mazingira kama hayo.
Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa hapa jijini Tehran amepongeza maandamano ya mamilioni ya Wairani ya Disemba 30 mwaka 2009 yaliyofanyika kwa lengo la kuonyesha uungaji mkono wao kwa mfumo wa Kiislamu na viongozi wake akiwemo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei. 925543


captcha