Kwa mujibu wa televisheni ya al-Jazeera, Wamisri hao walifanya maandamano hapo siku ya Alkhamisi mara tu baada ya kutolewa hukumu ya kuondolewa lawama watuhumiwa hao, ikiwa ni katika kulalamikia hatua hiyo na pia kuomboleza na familia za mashahidi na majeruhi wa mauaji hayo ya Januari 25.
Waandamanaji wamekosoa vikali utendaji wa Baraza la Kijeshi la Misri nchini humo na kutaka kisasi cha mauaji hayo kilipizwe mara moja dhidi ya watuhumiwa.
Mahakama ya Jinai ya Misri siku ya Alkhamisi iliyopita iliwaachilia huru maafisa watano wa polisi waliokuwa wakituhumiwa kuhusika na mauaji ya waandamanaji wa Misri mbele ya kituo cha polisi cha eneo la as-Sayyidatu Zeibab. Mahakama hiyo imedai kwamba polisi walichukua hatua ya kuwaua waandamanaji kama hatua ya kujilinda. 925535