IQNA

Hamasa ya 9 Dey, Harakati ya Kudumu Iran

11:20 - January 01, 2012
Habari ID: 2248796
Taifa la Iran Ijumaa tarehe 30 liliadhimisha mwaka wa pili wa Hamasa ya Tisa Dey. Katika miongo mitatu tokea ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu, kumekuwepo na siku muhimu na zenye taathira kubwa katika kuendeleza harakati ya kimapinduzi ya taifa la Iran. Hamasa ya Tisa Dey ni kati ya siku hizo muhimu.
Mnamo tarehe 9 Dey mwaka 1388 Hijria Shamhsia iliyosadifiana na Disemba 30 mwaka 2009 kulijiri tukio kubwa na la kihistoria nchini Iran ambalo lilikuwa jibu kwa mirengo potofu baada ya uchaguzi wa 10 wa rais nchini. Tukio hilo lilikuwa hamasa ya kudumu ya busara, ufahamu na mwamko wa taifa la Iran mbele ya njama na fitina za ndani na nje ya nchi. Uchaguzi wa rais wa Juni 2009 nchini Iran ulikuwa nukta muhimu katika uga wa uchaguzi nchini Iran. Asilimia 84 ya wapiga kura walishiriki Katika uchaguzi huo usio na kifani. Tukio hilo lililojiri wakati wa kuanza muongo wa nne wa Mapinduzi ya Kiislamu, liliashiria kuwa mfumo wa Kiislamu nchini Iran unamilikiwa na wananchi.Tukio hilo lilivuruga kabisa njama za Marekani za kuwachochea Wairani wasishiriki katika uchaguzi na kuitenga Iran kimataifa.
Aghalabu ya weledi wa mambo wanaamini kuwa kushiriki kwa wingi taifa la Iran katika uchaguzi wa Juni 2009 kungeweza kutoa pigo la mwisho kwa miradi mbalimbali ya nchi za Magharibi dhidi ya Iran. Lakini bada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi, hatua ya kupinga matokea ya uchaguzi ya baadhi ya wagombea urais ilivuruga hali ya kisiasa na kijamii ya Iran na kuzusha ghasia na machafuko. Harakati hii potofu ilidhamini matakwa ya madola ya Kimagharibi dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu. Ghasia hizo za mrengo wa fitina zilifika kileleni kwa kuvunjia heshima siku ya maombolezo ya Ashura katika mwezi wa Muharram. Lakini taifa la Iran, ambalo katika miongo mitatu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu limekuwa likijitokeza katika medani kila wakati utambulisho wa jamii na mfumo wa Kiislamu unapokumbwa na hatari, vilevile katika kipindi hicho nyeti lilijitokeza kwa pamoja katika maandamano ya mamilioni ya tarehe 9 Dey. Katika maandamano hayo, Wairani walilaani vikali mrengo potofu na kwa hatua hiyo wakaweza kuzima fitina ambayo ilikuwa inaongozwa kutoka nje ya nchi. Katika kipindi hicho ilibainika wazi kuwa Marekani na Uingereza zilikuwa zinaongoza fitina hiyo. Madola hayo ya kibeberu kupitia balozi za nchi za Magharibi mjini Tehran na mashirika ya kijasusi ya Kimagharibi, yalikuwa yakichochea fitina hizo kupitia idara maalumu nje ya Iran.
Harakati ya pamoja ya taifa la Iran mnamo tarehe 9 Dey kwa hakika ilionyesha kuwa wananchi wa Iran wako macho kabisa kwa ajili ya kulinda mapinduzi na kutetea thamani za mfumo na uongozi. Ni kwa sababu hiyo ndio maana Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei akautaja ushiriki huo wa kihistoria kwamba ni harakati iliyotokana na busara na kutambua hali.
Harakati ya Dey 9 kwa hakika iliashiria irada itokanayo na ufahamu wa taifa lote la Iran. Harakati hiyo ilionyesha kuwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu katika kukabiliana na vita vya kinafsi na changamoto nyeti za maadui ina rasilimali kubwa ambayo ni wananchi. Marekani Katika uhasama wake usio na kikomo na taifa la Iran katika miaka yote iliyopita hadi sasa imekuwa ikijaribu kuweka vikwazo kwa kisingizio cha ukiukaji wa haki za binadamu na madai yasiyo na msingi kuhusu kadhia ya nyuklia. Njama hizo za Marekani za kuitenga Iran zimekuwa zikigonga ukuta. Aidha njama za Marekani za kuingilia mambo ya ndani ya Iran zimeambulia patupu.
Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alibainisha wazi njama za Washington dhidi ya Iran pale alipohojiwa na BBC ya Kifarsi na kutangaza rasmi kuwa Marekani ilijaribu kuunga mkono mrengo wa fitina nchini Iran. Kwa hivyo tunaweza kusema kuwa Hamasa ya tarehe 9 Dey inapaswa kuzingatiwa kwa kina kwa mitazamo yote kama harakati ya kudumu ya kujitolea ya wananchi yenye athari za kudumu.
925386
captcha