Sheikh Ahmad Moballeghi, Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Kuyakurubisha Madhehebu ya Kiislamu amesema kumekuwepo na hitilafu na migongano katika historia ya ulimwengu wa Kiislamu lakini sasa wakati umefika kuangazia msingi wa Qur’ani wa umma mmoja.
Sheikh Ahmad Moballeghi alikuwa akizungumza Disemba 31 katika kikao cha ‘Maktaba ya Ashura na Ukuruba wa Madhehebu ya Kiislamu’.
Amesema pamoja na kuwa harakati ya Imam Hussein AS ina chimbuko la Kishia, lakini ilijiri katika umma wa Kiislamu na malengo yake yalikusudia kuunufaisha umma mzima wa Kiislamu.
Kuhusu sababu ya kukosekana umoja na ukuruba wa madhehebu ya Kiislamu, amesema katika karne kadhaa sasa kumekuwa na njama za kuzusha uhasama na mifakarano ya kimadhehebu.
Ameongeza kuwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran ulikuwa nukta muhimu katika kuleta ukuruba miongoni mwa madhehebu ya Kiislamu.
Sheikh Ahmad Moballeghi ametoa wito kwa Waislamu kuvumiliana na kuepuka mifarakano ili lengo la Qur’ani la ‘kuwepo umma mmoja’ liweze kufikiwa.
926288