Vyombo hivyo vinasema kuwa Adnan Mansur, Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon amekuwa akifanya mazungumzo ya simu na viongozi wa Libya ili kuandaa mazingira ya kufanyika safari hiyo nchini humo.
Waziri huyo anatazamiwa kuongoza ujumbe wa ngazi za juu wa kidiplomasia na usio wa kidiplomasia kwa lengo la kuchunguza hali ya hivi karibuni kabisa kuhusiana na hatima ya mwanazuoni huyo mashuhuri wa Lebanon na wenzake.
Wakati huohuo Hani al-Qubeisi, afisa mwandamizi wa chama cha Amal amesema kwamba habari zinazotangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusiana na hatima ya Imam Musa Sadr hazina ukweli wowote. Ameitaka serikali mpya ya Libya kuzima njama za vyombo hivyo vya habari kuhusiana na faili la Musa Sadr na kusaidia kupatikana njia za kumwezesha mwanachuoni huyo mashuhuri wa Kiislamu kurejea kwenye uwanja wa jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. 926280