IQNA

Mkristo aliyemvunjia heshima Mtume Misri ahukumiwa kifungo

15:17 - January 01, 2012
Habari ID: 2249250
Mwendesha mashtaka wa mkoa wa Asyut wa Misri amemhukumu kifungo cha siku nne jela Jamal Abduh Mas'ud, Mkristo wa Kikopti aliyepatikana na hatia ya kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) katika mtandano wa kijamii wa Facebook.
Mwendesha mashtaka Hamza Ibrahim wa mkoa wa Asyut amemhukumu adhabu ya kifungo cha siku nne Mkristo huyo kwa hatia ya kuvunjia heshima dini za mbinguni na kuchapisha picha za dharau dhidi ya Mtume (saw) na Waislamu katika mtandao wa Facebook.
Mkristo huyo alishiriki katika machafuko yanayohusiana na fitina za kidini zilizotokea katika mkoa wa Asyut na kuzusha ghasia kubwa katika vijiji vya Manqabad, al Adar, Bahiij na Salam. 926706


captcha