IQNA

Vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu vyaongezeka Uholanzi

10:18 - January 02, 2012
Habari ID: 2249545
Idhaa ya Uholanzi siku ya Jumamosi ilitoa ripoti inayoonyesha kwamba vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu vimeongezeka maradufu nchini humo na kwamba katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2010 kesi 117 za mashambulio dhidi ya misikiti ziliripotiwa.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Kuwait KUNA, idhaa hiyo imemnukuu mtaalamu mmoja wa masuala ya kijamii wa nchi hiyo akisema kwamba vitendo hivyo vimekithiri kutokana na kuongezeka chuki dhidi ya dini ya Kiislamu.
Kesi 43 kati ya hizo zinahusiana na uandishi wa maneno na alama za chuki na uadui dhidi ya Uislamu kwenye kuta za misikiti ambapo kesi 37 nyingine zinahusiana na kuharibiwa misikiti.
Katika kesi 99 polisi ya nchi hiyo imeshindwa kuwatambua wahusika wa vitendo hivyo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Nchini Uholanzi misikiti mingi imejengwa nje ya miji mikubwa. Kwa ujumla kuna misikiti 450 ambayo huwahudumia Waislamu wapatao milioni moja kati ya jamii ya watu milioni 16.5 wa nchi hiyo. 926881
captcha