Kanali ya televisheni ya kimataifa ya al Alam imeripoti kuwa, swala ya shukrani ilisali jana baada ya swala za Magharibi na Ishaa katika Msikiti wa Qaim mjini Beirut, Msikiti wa Bilal al Habashi mjini Baghdad na Msikiti wa Amirul Muuminin katika mji mtakatifu wa Najaf huko Iraq.
Swala ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kutokana na kuhitimishwa uvamizi wa Marekani nchini Iraq pia ilitekelezwa mjini Tehran katika misikiti ya Imam Mahdi (as), Hadhrat Abul Fadhl na Msikiti wa Chuo Kikuu cha Imam Swadiq (as). Katika mji mtakatifu wa Qum pia Waislamu waliswali swalatu Shukr katika Haram ya Bibi Maasuma (as).
Mkurugenzi wa Kamati ya Wananchi ya Kukumbuka Mashahidi wa Ulimwengu wa Kiislamu Muhammad Mahdi Rahimi amesema kuwa kuondoka askari vamizi wa Marekani nchini Iraq kutakuwa na matunda mengi kwa nchi hiyo.
Ameongeza kuwa kuhitimishwa uvamizi wa Marekani nchini Iraq sambamba na mwamko wa sasa wa Kiislamu katika Mashariki ya kati na kaskazini mwa Afrika ni ishara kwamba nchi zote za Kiislamu zinaweza kujiondoa katika makucha ya wavamizi kwa kuimarisha umoja na mshikamano wao. 927304