Akizungumza na IQNA, Ayatullah Mohammad Ali Taskhiri ameongeza kuwa: "Wazayuni awali walidhani matukio ya sasa Mashariki ya Kati yatakuwa kwa maslahi yao laini si hivyo. Netanyahu alinukuliwa akisema alikuwa na matumaini kuhusu mwamko katika nchi za Kiarabu lakini amegundua sasa kwamba mwamko huo ni kwa madhara ya Israe', amesema Ayatullah Taskhiri na kuongeza kuwa Wazayuni sasa wanafikiria njia za kujinusuru kupitia utendaji jinai.
Mwanazuoni huyo mwandamizi wa Iran amesema mwamko wa Kiislamu unatoa bishara njema kwa ulimwengu wa Kiislamu na kwamba umma wa Kiislamu hivi karibuni utaungana dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.
Ayatullah Taskhiri amesema kuwa Wazayuni awali walikusudia kuteka ardhi za Waislamu katika eneo lote kutoka Mto Nile hadi Mto Euphrates lakini ndoto yao hiyo iliambulia patupu kufuatia ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Intifadha ya Wapalestina na mwamko wa Kiislamu. Amesema Wazayuni sasa wanalazimika kuishi ndani ya ukuta wa kibaguzi.
Hivi karibuni Utawala wa Kizayuni wa Israel ulitangaza mpango wa kuutangaza mji mtakatifu wa Quds kuwa mji mkuu wa utawala huo ghasibu.
Mufti wa Quds huko Palestina amesema kuwa, mpango wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kuutangaza mji mtakatifu wa Quds kuwa mji mkuu wa utawala huo ghasibu ni batili na inayokinzana na sheria.
Sheikh Muhammad Hussein amesema, hata kama mpango huo utapasishwa na Bunge la utawala haramu wa Israel bado utakuwa batili na usiokubalika kwani umetoka kwa utawala vamizi unaozikalia kwa mabavu ardhi za Palestina.
Ismail Hania Waziri Mkuu wa serikali halali ya Palestina iliyochaguliwa na wananchi amesema kwamba, uamuzi huo wa Israel ni batili na kusisisitiza kwamba, Quds ni mji mkuu wa Palestina na daima ni kipenzi cha nyoyo za mamilioni ya Waislamu.
927367